Ep. 11 - Salama Na Ben Pol | WA MNYANG’ANGA
Katika pita pita zanguangu kwenye mitandao leo asubuhi nilikutana na video ya Ben Pol akiwa anaelekea kupanda zake helicopter na video ikamuonyesha akiwa anazunguka kwenye fukwe za huko alipokua na baadae ikaishia kwa kuonyesha watu wawili wakiwa wanaelea hewani... Mmoja wapo bila ya shaka alikua ni yeye, kuna mtu ambae amekua aki enjoy maisha yake miaka ya hivi karibuni kama yeye? Niko hapa nangoja jibu lako... na bila ya shaka mmoja wa watu hao wawili alikua ni yeye. Kutoogopa na kutimiza malengo aliyojiwekea ndo siri ya kukamilisha hesabu alizokua kapiga, na bila ya shaka baraka za Mwenyezi Mungu zinakamilisha yote. Kuna mtu ambae amekua eki enjoy maisha miaka ya hivi karibuni kama yeye? Niko hapa nangoja jibu lako… ???? Mpole, mcheshi, mwenye kusikiliza wakati mwengine akiwa anaongea, mwenye akili iliyo makini kwa umri wake na mpenda familia. Ben Pol amekuwa kwenye industry ya muziki wetu kwa miaka zaidi ya tisa sasa. Uhodari wake wa kuimba na kumiliki jukwaa vyema kabisa kitu ambacho ni adimu kwa waimbaji wanaofanya muziki wa aina yake, ila kwake yeye haikuwahi kuwa kazi ngumu toka siku ya kwanza alipokabidhiwa jukwaa, na kama unaniamini mimi, basi si jukwaa la muziki tu ndo amekua akilimudu uzi analoliweza kweli kweli, bali jukwaa la majukumu, la uandishi na hata ya uongozi. Amekua akipewa majukumu wakatia bado mdogo na aliweza kuyamiliki vizuri na matunda yake kuonekana mapema kabisa. Mzaliwa wa Dar es Salaam, na wakati anazaliwa Mzee wake hakua nyumbani na mazingira ambayo alizaliwa nayo yeye pekee ndo anaweza kutukhadithia na pengine kutokea huko na mazingira aliyokulia, aliyosomea, aliyoyapitia mpaka leo hii tunamfahamu ndo yamemfanya awe aina ya mtu aliye leo. Tushawaona watu wengi wakiwa wanabadilika mara tu baada ya kupata umaarufu. Simu zikawa hazipokelewi tena, pengine hata namba kubadilishwa, marafiki kubadilika, uchelewaji wa kwenye interview na kazi ikawa jambo la kawaida, marafiki wa kike kujaa kwenye phonebook na mambo mengine ya kukera, ila si kwa kwake yeye. Ameweza kutenganisha ukweli kwamba yeye ni mwanamuziki mkubwa na hodari ambae anawafurahisha wengi lakini pia ni mwana tu ambae ni mtoto kwa wazazi wake wapendwa na Kaka kwa mdogo wake, Baba kwa Mali na bila ya shaka mchumba kwa Anerlisa. Kwahiyo kitu gani haswa kimemfanya awe makini kwenye mambo yake na maamuzi anayofanya? Unadhani yeye ndo mwanamuziki mwenye vokali noma zaidi hapa kwetu? Au pengine ndo muimbaji anajielewa zaidi? Kipi kinampa hiyo nguvu ya kuwa humble kuweza kunyosha mambo yake kama yamepimwa kwa rula? Well… Majibu yako humu kwenye haya maongezi yangu naye. Kutoka kuzaliwa nyumbani kwa msaada ya jirani akiwa na Mama tu, maisha ya ujana ya Baba yake, mtihani walioupata kama familia baada ya kutokea kifo ndani ya nyumba yao, alipokua mdogo alikua mwanafunzi wa aina gani, na khadithi za mtoto wake. Tulikua na uwanja mpana wa mazungumzo na kilichozungumzwa kitakusaidia kukupeleka sehemu flani. Enjoy. Love, Salama Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support