Ep. 9 - Salama Na Khadija Kopa | ALIYEPEWA KAPEWA
Khadija Omar Kopa. Malkia wa mipasho na lejendari wa muziki wa Taarab kwenye ukanda huu na duniani kwa ujumla, mwenyewe kaniambia yeye kwenda Arabuni na Ulaya ni jambo la kawaida tu kwake maana hayo kayaanza kuyafanya kitaaambo sana. Kitambo kweli naweza sema, mimi nimeanza kumfahamu Da Khadija toka kigori kabisa, na amekua hapo kwenye standard hiyo hiyo kwa miaka nenda na miaka rudi. Hii bila ya shaka imetokana na kwamba na yeye alianza kufanya hizo kazi akiwa bado msichana mbichi kabisa. Na ameweza kutuliza akili yake na ku maintain standard na status yake kwa miaka nenda miaka rudi kitu ambacho ni kigumu kwa mwanamke, tena kwa mwanamke wa visiwani ambako miongozo ya kidini ina mizizi kama ya mbuyu lakini ameweza kutunza heshima yake na kuonyesha kipaji chake huku akiwa na staha yake. Inabidi uwe na nguvu ya ziada kuweza kuwa na ujasiri wa aina hiyo. Bila ya shaka alikua pia akipambana na mengi, pengine kukatishwa tamaa au hata vitisho ili aache kufanya alichokua anafanya kwa kutumia kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu lakini wapi, kwa mbwembwe za hali ya juu yeye ndo ameibuka kidedea kwenye vita hiyo na ndo maana heshima ya ulejendari inamhusu moja kwa moja Dada yangu huyu. Wengine watasema pengine yeye si muimbaji wa taarab mwenye sauti nzuri zaidi ya flani na fulani, pengine kuna ukweli ndani yake, lakini je, hao wenye hizo sauti nzuri zaidi yake wako wapi? Je wana uwezo wa kucheza na kuringa jukwaani kama Khadija Kopa? Je wanajulikana kama yeye? Je wana ushirikiano na wana muziki wa kizazi kipya cha Bongo Flava na kutoa nao nyimbo zilizoshika chati ya juu? Je wana uwezo wa kuingiza Taarab yao kwenye matamasha ya muziki wa kizazi kipya na watu waka bang kama kawa? Mimi na wewe tunajua jibu. Hii ni kwa ajili ya Dada yangu, fundi wa hizi kazi, tumpe heshima yake maana ‘Mpewa hapokonyeki, aliyepewa kapewa...’ Tafadhali Enjoy. Love, Salama. Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support