Ep. 4 - Salama Na Barnaba | FUNDI

Barnaba ni mfupi (siko hapa kumtoa kasoro) ila wazungu wana usemi wao ambao nitausema kwa kiswahili, ya kwamba vitu vizuuuri huja kwenye pakeji ndogo. Ukitaka kuelewa maana yake kama hujang’amua basi kamuulize Bibi. Umbo lake na uwezo havifanani , na kama ingekua ubora na kipaji ndo ukubwa wa mwili basi mwenzetu angekua kama HERCULES, pia siko hapa kwaajili ya kumtukuza bali kusema vile nimunavyo katika macho yangu. Ni kijana ambaye anajifunza kila siku iendayo kwa Mungu, hajawahi kujikweza, mwenye roho ya Imani, mwenye kumuogopa Mungu na pia asiyesahau alipotoka na pia alotoka nao huko alipotoka. Mtanashati pia, na ukiniuliza mimi naamini kabisa hiki ni kitu ambacho kimekua kikistawi kwa siku zinavyokwenda, na huo ndo ukuaji, maana kukua si nywele na kucha tu, hata kujielewa na kufahamu kwamba nyanya pia ni tunda lakini juisi yake mpemba hauzi pia ni ukuaji. Muziki ndo mpenzi wake wa kwanza, ambao umemuepusha na mengi na kumpa vingi pia na kumkutanisha na watu ambao pengine alikua anawaona kwenye picha tu, kuufahamu kwake mziki kwa kujifunza kupiga gitaa na kuutengeneza kama muandaaji na pia kuweza kuuandika ni kipaji ambacho Jalali kampatia, na jinsi ambavyo si mchoyo wa kuwapa na wenzie wakang’ara (kitu ambacho alijifunza) ndo ambacho pia kinampa utofauti kati yake na wengine wengi. Kwenye kikao hiki mimi naye tulianzia nyuma kiasi, enzi za kuokota vyuma chakavu ili mambo yaende, kupigiwa kelele ya mwizi na kuponea chupuchupu kuchezea kibiriti, THT, uandishi, heshima, Marehemu Ruge, maisha ya ndoa, social media na mengine ya kutosha. Ilikua siku ya kujifunza mengi kutoka kwake na kwa hilo namshkuru Mungu kwa kunikutanisha nae. Tafadhali Enjoy. Love, Salama --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232