Ep. 1 - Salama Na Lil Ommy | AIR TABORA

2016 ndo mwaka nilikutana na Lil Ommy mara ya kwanza, pengine nilishawahi kukutana naye huko nyumba ila sikumbuki. Aliniomba niende kwenye kipindi chake cha The Playlist enzi hizo kikiwa Jumamosi asubuhi ya tarehe 20 mwezi wa nane. Sikuwahi kupenda kufanyiwa interview ila siku hiyo nilimpa Ommy nafasi, sikuwahi kujutia na pengine hiyo ndo sababu ya kumfanya yeye awe mgeni nambari moja kwenye Podcast hii. Anayejitambua, anayejituma, anayesoma, mwenye nia na mipango endelevu… Nilimuomba aje na hapa tulizungumza karibia yote. Ya kwao Tabora, familia yao, marehemu Mzee wake, marehemu Dada yake, ndugu zake wa kambo, utundu wa udogoni, kutafuta kazi, maisha ya mjini na marafiki, muziki wa kizazi kipya na ushindani wa kazi. Times FM na siku ya harusi yake. Na hakua mchoyo wa kunikhadithia. Hii ni kwa ajili yako, na nyengine nyingi zijazo zinakuhusu pia. Chukua baadhi ya kurasa kwenye kitabu cha AIR TABORA na tumia baadhi ya aliyoyoyasema kuboresha kitabu chako maana nami nafanya hivyo. Enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

牛油果烤面包

Tobi Johnson a Jennifer Bennett: Volunteer management experts

الشيخ بسام جرار

The Health Code

Sleep Sounds by TMSOFT

Harshita Pailani

Nedsir

Swasthik and Srikrishna