MSINIHUSISHE NA SIASA ZA OBADO, ASEMA HELLEN
Mkewe gavana wa Migori Bi. Hellen Adhiambo ambaye pia anawania kiti cha mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Migori amewataka wapinzani wake wawache kumtwika mzigo wa kuhusisha siasa zake na gavana huyo anayeondoka akisema yakwamba yeye ni mwaniaji wa kiti hicho kama wawaniaji wengine.