UTUMIZI MBAYA WA E-PILLS NA MADHARA YAKE
Baadhi ya mashirika hapa nchini yamekuwa katika mstari wa mbele wakuhamasisha wananchi kuhusu mbinu na njia mbali mbali za kupanga uzazi.Mchakato huo wote unatarajiwa kuzuia kupatikana kwa mimba za mapema na zisizotarajiwa, hatua ambayo imechangia pakubwa utumizi wa vidonge vya kuzuia mimba za dharura almarufu E-Pills. Karibu kwa Makala haya yanayoangazia kwa kina athari za utumizi mbaya wa dawa za kupanga uzazi hususan vidonge vya E- PILLS