MAKALA: NDUGU HASIMU MPAKANI
Kwa miaka na mikaka jamii ya wakuria wanaoishi mpakani mwa Kenya na Tanzania wameishi kama Ndugu. Lakini visa vya hivi majuzi vya wakuria kutoka upande Wa Kenya kuvamiwa nchini Tanzania wanapovuka mpaka kuingia katika taifa hilo jirani vinatishia kusambaratisha undugu kati ya jamii hiyo inayotenganishwa na mpaka.